December 31, 2009

Mh. Rashid Mfaume Kawawa afariki dunia. 1926-2009


Simba wa vita Mh. Rashid Kawawa amefariki dunia leo mapema katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. Marehemu kawawa aliwahi kutumikia ngazi mbalimbali katika taifa letu kwa kushika nafasi ya uwaziri mkuu wa kwanza. Mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen

December 24, 2009

wapendwa krismas njema

Leo ikiwa ni siku ya mkesha wa sikukuu ya kuzaliwa kwa bwana yesu kristo ambapo wakristo huitumia siku hii kwa kuwa makanisani basi napenda kuwatakia mkesha mwema kwa kitafakari yale yote yanayompendeza bwana.

December 18, 2009

Hepi bethi dei Khalid Kalema


Wana Hindoo family kwa niaba ya wana Coast family-tawi la mlimani city wanakutakia maisha marefu yenye furaha.

December 14, 2009

Hongera Paulina Nkini


Familia ya bwana na bibi Bendera wanakupongeza sana kwa kupata kipaimara chako.Tunakutakia maisha mema katika maisha yako.

kutoka kulia ni baba mzazi wa Paulina Nkini


keki ya asili ilikuwapo siunajua tena kutoka kule kwetuu.....

December 10, 2009

miaka 48 ya uhuru

Miaka 48 ya uhuru wa Tanganyika yameadhimishwa jana katika uwanja wa uhuru huku kauli mbiu ikisema tulinde na kuudumisha umoja wetu. Katika sherehe hizo zilizoongozwa na amir jeshi mkuu Dk. Jakaya Mrisho kikwete huku mamia ya watanzania wakishuhudia. Viongozi wengine walio hudhuria ni Rais wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, waziri kiongozi wa Zanzibar, rais mstaafu wa awamu ya pili Hassani Mwinyi na viongozi mbalimbali toka kambi ya upinzani. Mungu ibariki Tanzania.

November 26, 2009

MITANDAO YA SIMU NA SOKO LA AJIRA

Katika kipindi cha hivi karibuni tumeshuhudia huduma za mitandao ya simu kuimarika kwa kiasi kikubwa hata kufanya huduma hiyo kuwafikia watumiaji wengi hapa nchini. Katika kuhakikisha matumizi ya huduma hiyo nyeti inawafikia walengwa kwa ubora wa juu makampuni yaliyo mengi nayo yamejikita katika kuhakikisha yanakwenda sambamba na soko la ushindani. katika hili wanastahili pongezi lakini kilichonifanya kuandika hiki ni juu ya makampuni haya kujihusisha na huduma za kifedha ambapo hapo awali zilikuwa zikifanywa na taasisi za kibenki. Wasiwasi wangu ni juu ya soko la ajira katika mabenki  ambalo ndilo soko tegemezi  kwa kiasi kikubwa kwa kuajiri watu wengi hususani wanafunzi pindi wamalizapo masomo yao vyuoni. Sasa kama huduma hii ya simu za mkononi itaweza kuwafikia watumiaji wa huduma hiyo kwa uhakika ina maana kuwa ajiri ya wafanyakazi walio katika taasisi za kifedha kama mabenki wakijikuta wanapoteza ajira zao. lakini je makampuni ya simu yamejiaandaa kukabiriana na wateja wao wote? Tunasikia kuwa makampuni hayo ya simu yanajianda katika kuhakikisha wafanyakazi wanapokea mishahara yao kupitia njia ya simu.Je usalama utakuwa je?

November 23, 2009

KUPIGA KELELE MWISHO UMBALI WA MITA 30

Nchini Kenya tume inayohusiana na mazingira  inatarajia kupitisha sheria  inayokataza kupiga kelele kwa umbali usiozidi mita 30 kutoka pale ulipo.Katika kuhakikisha kuwa sheria hiyo inafaatiliwa tume hiyo imetangaza kuwatoza faini ya ksh 30,000 au kwenda jela kwa miezi 18. Sheria hii itawakabiri wapiga debe, waumini wa dini za kilokole,  kumbi za starehe ambazo sauti zake zimekuwa zikiwabughudhi wananchi. Swali ni je itafanikiwa?

November 20, 2009

Maadhimisho ya miaka kumi ya jumuiya Ya Afrika Mashariki

Maadhimisho ya miaka kumi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanaendelea mjini Arusha ambapo Marais wa nchi 5 yaanai Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya na mwenyeji Tanzania. Katika kuadhimisha siku hiyo kutakuwapo na uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa makao makuu ya jumuiya hiyo.

November 12, 2009

Wiki mbili za matatizo TZ

Ni takribani wiki mbili sasa tangu mwezi huu kuanza na kushuhudia majanga na matukio mbalimbali kulikuta taifa letu la Tanzania. ajali za moto pale Maisha Klabu, kufungiwa kwa mitambo ya Dowans na maporomoko ya udongo huko Same na ajali mbalimbali za vyombo vya barabarani

October 31, 2009

SIMBA KIDEDEA


Simba SC yairarua Dar Young African watoto wa jangwani kwa bao moja bila lililofungwa kimyani na Musa Mgosi na hivyo kuweka rekodi yakutopoteza mechi hata moja katika mzunguko wa kwanza.

Jahazi yazindua daktari wa mapenzi








mashabiki wakiramba arambaa arambaaaa.....




Jahazi modern taarab chini ya bingwa wa mapenzi Mzee Yusuf imezindua albamu ya tano inayokwenda kwa jina la DAKTARI WA MAPENZI katika ukumbi wa diamond Jubilee. Hakika mapenzi yalipata daktari kwani mashabiki walikongwa roho zao kisawasawa......

October 27, 2009

wafungaji bora duniani

ANTONIO DI NATALE UDINESE 9 SERIE A
ANDERSON NENE MONACO 9 LIGUE 1
JOHN BOKO AZAM FC 8 VODACOM Tanzani
DIDIER DROGBA CHELSEA 8 PREMIER LEAGUE
FERNANDO TORRES LIVERPOOL 8 PREMIER LEAGUE
HUSSEIN BUNU JKT RUVU 7 VODACOM Tanzania
WAYNE ROONEY MAN UTD 6 PREMIER LEAGUE
CRISTIANO RONALDO REAL MADRID 5 LA LIGA

October 25, 2009

raha ya koko bichi

Koko bichi ni moja ya fukwe maarufu kwa wakazi wengi wa jijini Dar kwa wananchi wengi kwenda kupumzika na kubadilishana mambo mawili matatu. Hapa pamekuwa ni moja ya maeneo maarufu kwa upatikanaji wa mix, mishikaki, mihogo n.k

October 24, 2009

SIMBA 1 AZAM 0

Simba SC yadhihilisha ubabe wake kwa Azam FC kwa kuichapa bao moja bila katika uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam

in reference to: Google (view on Google Sidewiki)

October 23, 2009

simba zaidi ya Manchester united



Simba sports club imeonyesha kuwa iko juu zaidi ya manchester united ya nchini uingereza kwa kuweza kufikisha point 24 ikiwa imecheza mechi 8 bila ya kupoteza mechi hata moja huku manchester wakiwa na point 22 na mchezo mmoja mbele ya simba. Wakati simba inakutana tarehe 31 oct na watani wao Yanga, manchester nao watakuwa na kazi ngumu ya kukutana na Liverpool jumapili ya tarehe 24 oct. Nani kati yao ataibuka mshindi?

October 19, 2009

Nafasi kwa mtoto



katika maisha ya sasa haya tuliyonayo mtoto anahitaji sana nafasi ya kuweza kujifunza mambo mbalimbali na hapo ndipo utakapoweza kutambua kipaji alichonacho kama mzazi juu ya mtoto wako. Hili bado halijawa jambo rahisi kwetu watanzania tukidhani kuwa hayo ni kwa wenzetu wazungu. Ninachoweza sema juu ya hili ni kwamba kila mzazi anayohaki yakumpatia mtoto wake malezi yaliyo bora ili mradi tu hayaendi kinyume na maadili ya malezi kwa mtoto.

Fukwe zetu









Hakika fukwe zetu zinamuonekano mzuri na wakuvutia.

October 14, 2009

Mwanza yaweka rekodi


Kwa mara nyingine tena Jiji la Mwanza laweka historia nyingine baada ya kijana Pascal Cassian kujinyakulia taji la BSS 3 na kujipatia kitita cha Tsh 25mil na kuwaangusha vinara wawili Peter Msechu kutoka Kigoma na Kelvin Mbati kutoka jiji la Lukuvi Dar Es Salaam. Ikumbukwe pia Miss Tanzania 2009 anatokea huko.

October 13, 2009

miaka 10 bila ya Mwl. J. K. Nyerere



Ni miaka kumi tangu mwl. J. K. Nyerere mwanzilishi wa taifa letu kututoka. Ni siku ya tarehe 14.10.1999 ndipo taifa lilipotwa na mshituko wa aliyekuwa baba wa taifa letu kipenzi cha watu kuwa ameaga dunia. Maswali mengi yalikuja vichwani mwa walio wengi juu ya namna taifa letu changa litakavyokuwa bila yeye. Japo mambo mengi aliyoyatabiri kuwa yatatokea kama yasiposhughulikiwa ndio yamejitokeza mfano ulimbikiziaji wa mali na mgongano wa kisiasa wa Zanzibar na mengine mengi. Imekuwa ni jadi yetu kama taifa kumkumbuka kila ifikapo tarehe 14. Je yale aliyoyaacha yanafuatwa? Viongozi wanakumbuka miiko ya uongozi? Mungu ilaze mahali pema roho yake amen.

Pregnant Woman Pregnant Again, Julia Grovenburg Conceives Consecutively - ABC News

facebook
Stephen Bendera
9:45am Oct 13th
Pregnant Woman Pregnant Again, Julia Grovenburg Conceives Consecutively - ABC News
To stezuvehra.1977@blogger.com
 
pregnant woman pregnant again

Stephen has shared a link to a news story with you. To view the news story or to reply to the message, follow this link:

http://www.facebook.com/p.php?i=1085725357&k=Z6MY53RXPYTF6BD1QAWXYUWQ2RIB4XZ1QWCPA&oid=1064566433891
If you do not wish to receive this type of email from Facebook in the future, please click here to unsubscribe.
Facebook's offices are located at 1601 S. California Ave., Palo Alto, CA 94304.

October 12, 2009

Hepi bethidei Paul Amani Bendera




Familia ya bwana na bibi Edward Paul Amani wa Lugalo wanayofuraha ya kumpongeza mtoto wao kipenzi Paul kwa kutimiza mwaka mmoja. Tunakutakia afya njema na makuzi mema.

October 09, 2009

Nobel Peace Price


Rais Barack Obama wa marekani ametunukiwa tuzo ya amani ya Noble Peace Price 2009 ikiwa ni muda mfupi tu tangu kuingia kwake madarakani.

October 08, 2009

Afya ya JK iko bomba


Madaktari wa rais J.K wathibitisha kuwa rais yuko fit katika kulitumikia Taifa letu la Tanzania.

October 07, 2009

Rais Jakaya Kikwete atimiza miaka 59


Tunakutakia birthday njema na afya tele katika kuliendesha taifa letu la Tanzania kwa amani na mshikamano.

October 05, 2009

mgao wa umeme



Mgao wa umeme ulionza hivi karibuni wawa chanzo cha kuzorota kwa kipato kwa wananchi hasa wakipato cha chini kutokana na shughuli za uendeshaji uchumi kusimama. Misongamano ya magari nayo yawa kero kwa watumiaji wa magari jijini. 

October 04, 2009

usiku wa maraha




Hapa Babu njenje akiimba wimbo wa kisebu sebu unaopendwa sana na wadau wa njenje

Nyota Waziri akiimba wimbo wa gere na staili ya kijoti joti hakika hapatoshi



anko Kitime akicharaza gita

Kwa raha kamili kutana uso kwa uso selender bridge kila siku ya Jumamosi

October 03, 2009

MIRIAM GERALD NDIYE VODACOM MISS TANZANIA 09


Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu hatimaye Miriam Gerald toka kanda ya ziwa atwaa taji la vodaacom miss Tanzania 2009 na kujinyakulia gari aina ya Grand vitara na pesa taslimu mil 9.

October 02, 2009

HOMA YAZIDI KUPANDA MISS TANZANIA

Homa yazidi kuwapanda warembo wanoawania taji la Vodacom miss Tanzania litakalofanyika mapema leo hii katika ukumbi wa kisasa wa mlimani city, jijini Dar Es Salaam. Mshindi kujinyakulia gari aina ya suzuki Grand lenye thamani ya sh mil. 53.2 na fedha taslimu sh mil 9.

NANI KUCHEKA KASEBA AU FRANCIS CHEKA?

LEO NDIO LEO SIKU ILIYOKUWA IKISUBIRIWA NA WADAU WENGI WAPENDAO MCHEZO WA NGUMI NCHINI KATI YA BINGWA WA MABARA WA KICKBOXING JAPHET KASEBA NA FRANCIS CHEKA ANAYESHIKILIA UBINGWA WA DUNIA WA ICB. MPAMBANO HUO UTAKAOKUWA WA RAUNDI 12 UTAFANYIKA KATIKA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM.

September 30, 2009

MAGAZETINI LEO


Waziri mkuu wa zamani, Dr Salim Ahmed Salim amesema kuwa wanachama wa chama cha mapinduzi wanaotaka kugombea uraisi sambamba na  Jakaya Kikwete waachwe wapambane naye, huku akionya kuwa hawatamuwe





 Jaji Joseph Sinde Warioba amemuonya rais Jakaya Kikwete katika kuzungumzia maswala ya kesi za EPA ambazo bado hazijafikishwa mahakamani kuwa kunaweza kumshushia hadhi yake.










waziri mkuu wa zamani, jaji Joseph Warioba ameonyesha wasiwasi wake kuhusu uongozi wa nchi, akisisitiza kuwa umekuwa karibu mno na matajiri, na nchi matajiri zaidi, kuliko wananchi wa kawaida.