August 20, 2010

Hongera LYDIA BENDERA

Tunapenda kukupongeza sana sisi kama wanafamilia kwa kuweza kurudisha fomu zako na kuweza kupitishwa jina lako bila ya kupingwa. Hakika mwenyezi mungu yu pamoja nawe katika harakati hizi za kisiasa katika kuweza kuja kuwawakilisha vyema wapiga kura wako wa jimbo la Kibaha Mjini. Tunafahamu kuwa safari ni ngumu katika kuhakikisha ndoto zako zinakuwa lakini kwa uweza wake mola yote yatakuwa sawa. Hongera sana tena sana

August 16, 2010

Bi Bendera kupeperusha bendera ya CUF

Safari ni hatua wahenga walisema na ndivyo ilivyoanza kwa Bi. Lydia Bendera katika kinyang'anyiro cha kugombea ubunge katika jimbo la Kibaha Mjini huku akipeperusha bendera ya CUF. Kila rakheri katika harakati hizo.