October 31, 2009
SIMBA KIDEDEA
Simba SC yairarua Dar Young African watoto wa jangwani kwa bao moja bila lililofungwa kimyani na Musa Mgosi na hivyo kuweka rekodi yakutopoteza mechi hata moja katika mzunguko wa kwanza.
Jahazi yazindua daktari wa mapenzi
mashabiki wakiramba arambaa arambaaaa.....
October 27, 2009
wafungaji bora duniani
ANTONIO DI NATALE UDINESE 9 SERIE A
ANDERSON NENE MONACO 9 LIGUE 1
JOHN BOKO AZAM FC 8 VODACOM Tanzani
DIDIER DROGBA CHELSEA 8 PREMIER LEAGUE
FERNANDO TORRES LIVERPOOL 8 PREMIER LEAGUE
HUSSEIN BUNU JKT RUVU 7 VODACOM Tanzania
WAYNE ROONEY MAN UTD 6 PREMIER LEAGUE
CRISTIANO RONALDO REAL MADRID 5 LA LIGA
ANDERSON NENE MONACO 9 LIGUE 1
JOHN BOKO AZAM FC 8 VODACOM Tanzani
DIDIER DROGBA CHELSEA 8 PREMIER LEAGUE
FERNANDO TORRES LIVERPOOL 8 PREMIER LEAGUE
HUSSEIN BUNU JKT RUVU 7 VODACOM Tanzania
WAYNE ROONEY MAN UTD 6 PREMIER LEAGUE
CRISTIANO RONALDO REAL MADRID 5 LA LIGA
October 25, 2009
raha ya koko bichi
Koko bichi ni moja ya fukwe maarufu kwa wakazi wengi wa jijini Dar kwa wananchi wengi kwenda kupumzika na kubadilishana mambo mawili matatu. Hapa pamekuwa ni moja ya maeneo maarufu kwa upatikanaji wa mix, mishikaki, mihogo n.k
October 24, 2009
SIMBA 1 AZAM 0
Simba SC yadhihilisha ubabe wake kwa Azam FC kwa kuichapa bao moja bila katika uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam
in reference to: Google (view on Google Sidewiki)October 23, 2009
simba zaidi ya Manchester united
Simba sports club imeonyesha kuwa iko juu zaidi ya manchester united ya nchini uingereza kwa kuweza kufikisha point 24 ikiwa imecheza mechi 8 bila ya kupoteza mechi hata moja huku manchester wakiwa na point 22 na mchezo mmoja mbele ya simba. Wakati simba inakutana tarehe 31 oct na watani wao Yanga, manchester nao watakuwa na kazi ngumu ya kukutana na Liverpool jumapili ya tarehe 24 oct. Nani kati yao ataibuka mshindi?October 19, 2009
Nafasi kwa mtoto
October 14, 2009
Mwanza yaweka rekodi
Kwa mara nyingine tena Jiji la Mwanza laweka historia nyingine baada ya kijana Pascal Cassian kujinyakulia taji la BSS 3 na kujipatia kitita cha Tsh 25mil na kuwaangusha vinara wawili Peter Msechu kutoka Kigoma na Kelvin Mbati kutoka jiji la Lukuvi Dar Es Salaam. Ikumbukwe pia Miss Tanzania 2009 anatokea huko.
October 13, 2009
miaka 10 bila ya Mwl. J. K. Nyerere
Ni miaka kumi tangu mwl. J. K. Nyerere mwanzilishi wa taifa letu kututoka. Ni siku ya tarehe 14.10.1999 ndipo taifa lilipotwa na mshituko wa aliyekuwa baba wa taifa letu kipenzi cha watu kuwa ameaga dunia. Maswali mengi yalikuja vichwani mwa walio wengi juu ya namna taifa letu changa litakavyokuwa bila yeye. Japo mambo mengi aliyoyatabiri kuwa yatatokea kama yasiposhughulikiwa ndio yamejitokeza mfano ulimbikiziaji wa mali na mgongano wa kisiasa wa Zanzibar na mengine mengi. Imekuwa ni jadi yetu kama taifa kumkumbuka kila ifikapo tarehe 14. Je yale aliyoyaacha yanafuatwa? Viongozi wanakumbuka miiko ya uongozi? Mungu ilaze mahali pema roho yake amen.
Pregnant Woman Pregnant Again, Julia Grovenburg Conceives Consecutively - ABC News
| ||||||
October 12, 2009
Hepi bethidei Paul Amani Bendera
Familia ya bwana na bibi Edward Paul Amani wa Lugalo wanayofuraha ya kumpongeza mtoto wao kipenzi Paul kwa kutimiza mwaka mmoja. Tunakutakia afya njema na makuzi mema.
October 09, 2009
Nobel Peace Price
Rais Barack Obama wa marekani ametunukiwa tuzo ya amani ya Noble Peace Price 2009 ikiwa ni muda mfupi tu tangu kuingia kwake madarakani.
October 08, 2009
October 07, 2009
Rais Jakaya Kikwete atimiza miaka 59
Tunakutakia birthday njema na afya tele katika kuliendesha taifa letu la Tanzania kwa amani na mshikamano.
October 05, 2009
mgao wa umeme
Mgao wa umeme ulionza hivi karibuni wawa chanzo cha kuzorota kwa kipato kwa wananchi hasa wakipato cha chini kutokana na shughuli za uendeshaji uchumi kusimama. Misongamano ya magari nayo yawa kero kwa watumiaji wa magari jijini.
October 04, 2009
usiku wa maraha
Hapa Babu njenje akiimba wimbo wa kisebu sebu unaopendwa sana na wadau wa njenje
Nyota Waziri akiimba wimbo wa gere na staili ya kijoti joti hakika hapatoshi
anko Kitime akicharaza gita
Kwa raha kamili kutana uso kwa uso selender bridge kila siku ya Jumamosi
October 03, 2009
MIRIAM GERALD NDIYE VODACOM MISS TANZANIA 09
Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu hatimaye Miriam Gerald toka kanda ya ziwa atwaa taji la vodaacom miss Tanzania 2009 na kujinyakulia gari aina ya Grand vitara na pesa taslimu mil 9.
October 02, 2009
HOMA YAZIDI KUPANDA MISS TANZANIA
Homa yazidi kuwapanda warembo wanoawania taji la Vodacom miss Tanzania litakalofanyika mapema leo hii katika ukumbi wa kisasa wa mlimani city, jijini Dar Es Salaam. Mshindi kujinyakulia gari aina ya suzuki Grand lenye thamani ya sh mil. 53.2 na fedha taslimu sh mil 9.
NANI KUCHEKA KASEBA AU FRANCIS CHEKA?
LEO NDIO LEO SIKU ILIYOKUWA IKISUBIRIWA NA WADAU WENGI WAPENDAO MCHEZO WA NGUMI NCHINI KATI YA BINGWA WA MABARA WA KICKBOXING JAPHET KASEBA NA FRANCIS CHEKA ANAYESHIKILIA UBINGWA WA DUNIA WA ICB. MPAMBANO HUO UTAKAOKUWA WA RAUNDI 12 UTAFANYIKA KATIKA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM.
Subscribe to:
Posts (Atom)

