November 26, 2009

MITANDAO YA SIMU NA SOKO LA AJIRA

Katika kipindi cha hivi karibuni tumeshuhudia huduma za mitandao ya simu kuimarika kwa kiasi kikubwa hata kufanya huduma hiyo kuwafikia watumiaji wengi hapa nchini. Katika kuhakikisha matumizi ya huduma hiyo nyeti inawafikia walengwa kwa ubora wa juu makampuni yaliyo mengi nayo yamejikita katika kuhakikisha yanakwenda sambamba na soko la ushindani. katika hili wanastahili pongezi lakini kilichonifanya kuandika hiki ni juu ya makampuni haya kujihusisha na huduma za kifedha ambapo hapo awali zilikuwa zikifanywa na taasisi za kibenki. Wasiwasi wangu ni juu ya soko la ajira katika mabenki  ambalo ndilo soko tegemezi  kwa kiasi kikubwa kwa kuajiri watu wengi hususani wanafunzi pindi wamalizapo masomo yao vyuoni. Sasa kama huduma hii ya simu za mkononi itaweza kuwafikia watumiaji wa huduma hiyo kwa uhakika ina maana kuwa ajiri ya wafanyakazi walio katika taasisi za kifedha kama mabenki wakijikuta wanapoteza ajira zao. lakini je makampuni ya simu yamejiaandaa kukabiriana na wateja wao wote? Tunasikia kuwa makampuni hayo ya simu yanajianda katika kuhakikisha wafanyakazi wanapokea mishahara yao kupitia njia ya simu.Je usalama utakuwa je?

November 23, 2009

KUPIGA KELELE MWISHO UMBALI WA MITA 30

Nchini Kenya tume inayohusiana na mazingira  inatarajia kupitisha sheria  inayokataza kupiga kelele kwa umbali usiozidi mita 30 kutoka pale ulipo.Katika kuhakikisha kuwa sheria hiyo inafaatiliwa tume hiyo imetangaza kuwatoza faini ya ksh 30,000 au kwenda jela kwa miezi 18. Sheria hii itawakabiri wapiga debe, waumini wa dini za kilokole,  kumbi za starehe ambazo sauti zake zimekuwa zikiwabughudhi wananchi. Swali ni je itafanikiwa?

November 20, 2009

Maadhimisho ya miaka kumi ya jumuiya Ya Afrika Mashariki

Maadhimisho ya miaka kumi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanaendelea mjini Arusha ambapo Marais wa nchi 5 yaanai Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya na mwenyeji Tanzania. Katika kuadhimisha siku hiyo kutakuwapo na uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa makao makuu ya jumuiya hiyo.

November 12, 2009

Wiki mbili za matatizo TZ

Ni takribani wiki mbili sasa tangu mwezi huu kuanza na kushuhudia majanga na matukio mbalimbali kulikuta taifa letu la Tanzania. ajali za moto pale Maisha Klabu, kufungiwa kwa mitambo ya Dowans na maporomoko ya udongo huko Same na ajali mbalimbali za vyombo vya barabarani