September 30, 2009

MAGAZETINI LEO


Waziri mkuu wa zamani, Dr Salim Ahmed Salim amesema kuwa wanachama wa chama cha mapinduzi wanaotaka kugombea uraisi sambamba na  Jakaya Kikwete waachwe wapambane naye, huku akionya kuwa hawatamuwe





 Jaji Joseph Sinde Warioba amemuonya rais Jakaya Kikwete katika kuzungumzia maswala ya kesi za EPA ambazo bado hazijafikishwa mahakamani kuwa kunaweza kumshushia hadhi yake.










waziri mkuu wa zamani, jaji Joseph Warioba ameonyesha wasiwasi wake kuhusu uongozi wa nchi, akisisitiza kuwa umekuwa karibu mno na matajiri, na nchi matajiri zaidi, kuliko wananchi wa kawaida.

September 29, 2009

CUF KUFANYA MAANDAMANO

CHAMA CHA WANANCHI CUF KESHO WANATARAJIWA KUFANYA MAANDAMANO YA AMANI KUELEKEA OFISI ZA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI. AKINUKURIWA LEO KUPITIA KITUO CHA TBC1 PRO. IBRAHIMU LIPUMBA AMESEMA KUWA WAMEAMUA KUFANYA MATEMBEZI HAYO ILI KUISHINIKIZA TUME YA UCHAGUZI KATIKA UANDIKISHAJI WA WANANCHI KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. MAANDAMANO HAYO YANATARAJIWA KUANZIA MAKAO MAKUU KUPITIA MTAA WA KONGO, MNAZI MMOJA KISHA KUPITIA POSTA HADI OFISI HIZO.

September 25, 2009

BOMU LAUA WATOTO WAWILI MBAGALA

WATOTO WAWILI WAMERIPOTIWA KUFARIKI DUNIA BAADA YA BOMU KULIPUKA KARIBU NA KAMBI YA JESHI LA WANANCHI (JWTZ), ILIYOPO MBAGALA KIZUIANI JIJINI DAR ES SALAAM. WATOTO HAO WAMETAMBULIKA KUWA NI REGINA CHAWELE (5) NA RAJAB SAID (6) AMBAO WALIKUWA WANACHEZA KARIBU NA BOMU HILO.

September 24, 2009

HUU NDIO UWANJA WETU


Katika majiji makubwa katika afrika mashariki Dar Es Salaam ni moja ya jiji kubwa lenye wakazi wengi wanaongezeka kila siku. Lakini katika kukabiriana na ongezeko la watu wengi katika miji jiji hili halijaweza kuchukua hatua muafaka za kukabiriana na ongezeko hilo hasa kwa kuongeza sehemu za kupumzikia. Katika kulizungumzia hilo imekuwa ni kero kwa abiria wasafirio ndani ya nchi na kwa wale wanaosafiri nje ya nchi kwa kutumia uwanja wetu wa kimataifa wa mwalimu Nyerere hasa pale ifikapo sikukuu za kidini mfano, eid pasaka na krismas kwa watoto kugeuza kuwa ni sehemu yao ya kutembelea. Inakuwa ni kelele kubwa sana na usumbufu kwa abiria na hivyo kusababisha usikivu hafifu kwa vipaza sauti vya uwanjani hapo kushindwa kusikika kwa kuwajulisha abiria ratiba mbali mbali. Napenda kuishauri serikali na uongozi wa uwanja kujabiri kuliangalia hili ili kupunguza tatizo hili.