September 24, 2009
HUU NDIO UWANJA WETU
Katika majiji makubwa katika afrika mashariki Dar Es Salaam ni moja ya jiji kubwa lenye wakazi wengi wanaongezeka kila siku. Lakini katika kukabiriana na ongezeko la watu wengi katika miji jiji hili halijaweza kuchukua hatua muafaka za kukabiriana na ongezeko hilo hasa kwa kuongeza sehemu za kupumzikia. Katika kulizungumzia hilo imekuwa ni kero kwa abiria wasafirio ndani ya nchi na kwa wale wanaosafiri nje ya nchi kwa kutumia uwanja wetu wa kimataifa wa mwalimu Nyerere hasa pale ifikapo sikukuu za kidini mfano, eid pasaka na krismas kwa watoto kugeuza kuwa ni sehemu yao ya kutembelea. Inakuwa ni kelele kubwa sana na usumbufu kwa abiria na hivyo kusababisha usikivu hafifu kwa vipaza sauti vya uwanjani hapo kushindwa kusikika kwa kuwajulisha abiria ratiba mbali mbali. Napenda kuishauri serikali na uongozi wa uwanja kujabiri kuliangalia hili ili kupunguza tatizo hili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

1 comment:
hii ndio bongo kila kitu kinakwenda kama kilivyo
Post a Comment