Hakika shirika la nyumba la Taifa chini ya bwana Mchechu wanastahili pongezi za dhati katika kuhakikisha wamekuja na mabadiliko makubwa na mauri katika kipindi kifupi. Ni dhahiri kubwa kuwa shirika lilikokuwa hapo awali si hapa lililopo hapa tena. Tunaweza ona jinsi shirika hilo lilivyokuwa likichelewa kukusanya makushanyo ya kodi toka kwa wapangaji wake na hivyo kulikosesha shirika mapato kwa wakati unaostahili. Leo tunashuhudia shirika likikusanya makusanyo yake ya kodi kwa wakati unaostahili. Kitu ambacho sijakielewa ni juu ya mradi mpya wa ujenzi wa makazi mapya ya shirika hilo likija na kampeni kabambe ya kuwezeshwa kukopa toka katika mabenki yaliyojihidhinisha na shirika la nyumba. Kiukweli kabisa ni kwamba idea ni nzuri lakini kwa jinsi ilivyoimekuwa ni ngumu sana kwa watanzania walio wengi kufaidika na mradi huo hasa ukizingatia watanzania tulio wengi hatukopesheki katika mataasisi haya ya kibenki. Mfano nyumba za shirika hilo zinauzwa kati ya Milioni 168 na unatakiwa kulipa malipo ya awali ya 10% na endapo utafanikiwa kupata nafasi kutokana na idadi ya watu walioomba utatakiwa kulipa salio lililobakia ndani ya siku 90 mara tu baada ya maombi yako kukubaliwa. Na kwa utaratibu jinsi ulivyo ni kana kwamba NHC watamalizana na benki husika kwa niaba yako kabla hata ya kipindi hicho kusudiwa kumalizika. Swali linakuja ni watanzania wangapi watakaoweza kunufaika na makazi bora toka katika shirika la nyumba hasa ukizingatia wengi wao hawapo katika ajira rasmi na hata walio na ajira rasmi kipato cha kukidhi marejesho ya benki. Hizi nyumba zimewakusidia akina nani?
May 09, 2012
February 11, 2012
Pongezi Kwa Wabunge
Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza wabunge wetu kwa uamuzi mzuri waliofikia katika kupitisha mswada wa sheria ya kuanda katiba mpya. Hakika wameonyesha uzalendo wa hali ya juu hasa kambi ya upinzani ambao tangu mwanzo walishaonyesha kutokuwa na imani kwa tume hiyo hadi kuwafikisha kwa Rais J.k. Napenda kuwapongeza kwa hatua nzuri waliyoifikia na kuendeleza amani na utulivu wa Taifa letu. Tumeweza shuhudia nchi nyingi hata hapa jirani zetu kutofikia muafaka mzuri katika kuhakikisha mambo ya katiba yanamalizika salama. Tunachowasihi viongozi wetu ni kuhakikisha mchakato wakupata maoni toka ngazi zilizohusishwa zinasimamiwa vizuri ili kutuepusha na matatizo yakuharibu amani hii tuliyonayo.
Subscribe to:
Posts (Atom)
