February 11, 2012

Pongezi Kwa Wabunge

Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza wabunge wetu kwa uamuzi mzuri waliofikia katika kupitisha mswada wa sheria ya kuanda katiba mpya. Hakika wameonyesha uzalendo wa hali ya juu hasa kambi ya upinzani ambao tangu mwanzo walishaonyesha kutokuwa na imani kwa tume hiyo hadi kuwafikisha kwa Rais J.k. Napenda kuwapongeza kwa hatua nzuri waliyoifikia na kuendeleza amani na utulivu wa Taifa letu. Tumeweza shuhudia nchi nyingi hata hapa jirani zetu kutofikia muafaka mzuri katika kuhakikisha mambo ya katiba yanamalizika salama. Tunachowasihi viongozi wetu ni kuhakikisha mchakato wakupata maoni toka ngazi zilizohusishwa zinasimamiwa vizuri ili kutuepusha na matatizo yakuharibu amani hii tuliyonayo.

No comments: