December 31, 2009

Mh. Rashid Mfaume Kawawa afariki dunia. 1926-2009


Simba wa vita Mh. Rashid Kawawa amefariki dunia leo mapema katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. Marehemu kawawa aliwahi kutumikia ngazi mbalimbali katika taifa letu kwa kushika nafasi ya uwaziri mkuu wa kwanza. Mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen

December 24, 2009

wapendwa krismas njema

Leo ikiwa ni siku ya mkesha wa sikukuu ya kuzaliwa kwa bwana yesu kristo ambapo wakristo huitumia siku hii kwa kuwa makanisani basi napenda kuwatakia mkesha mwema kwa kitafakari yale yote yanayompendeza bwana.

December 18, 2009

Hepi bethi dei Khalid Kalema


Wana Hindoo family kwa niaba ya wana Coast family-tawi la mlimani city wanakutakia maisha marefu yenye furaha.

December 14, 2009

Hongera Paulina Nkini


Familia ya bwana na bibi Bendera wanakupongeza sana kwa kupata kipaimara chako.Tunakutakia maisha mema katika maisha yako.

kutoka kulia ni baba mzazi wa Paulina Nkini


keki ya asili ilikuwapo siunajua tena kutoka kule kwetuu.....

December 10, 2009

miaka 48 ya uhuru

Miaka 48 ya uhuru wa Tanganyika yameadhimishwa jana katika uwanja wa uhuru huku kauli mbiu ikisema tulinde na kuudumisha umoja wetu. Katika sherehe hizo zilizoongozwa na amir jeshi mkuu Dk. Jakaya Mrisho kikwete huku mamia ya watanzania wakishuhudia. Viongozi wengine walio hudhuria ni Rais wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, waziri kiongozi wa Zanzibar, rais mstaafu wa awamu ya pili Hassani Mwinyi na viongozi mbalimbali toka kambi ya upinzani. Mungu ibariki Tanzania.