September 20, 2010

RUSHWA KUISHINDA NI KAZI

Nimekuwa ni kijaribu kufatilia harakati hizi cha uchaguzi mkuu kwa ngazi ya Rais, Ubunge na udiwani unaotarajiwa kufanyika siku chache zijazo. Katika kutazama huku na kule nimekuja kubaini kuwa siasa kwa nchi zetu hizi za ulimwengu wa tatu hasa hivi vyama vya upinzani kuja kuondoa serikali kuu itakuja kuwachukua miaka kama si karne kuhakikisha wanachukua nchi. Tumeweza ona vyama vingi vikitoka jasho katika kuhakikisha kuwa wanaweza kuwafikia wananchi kwa kuelezea sera zao. Lakini kadiri siku nazo zilizivyokuwa zikienda vya vipinzani vimejikuta vikiuza nafasi zao kwa siri na kukiachia chama tawala. Na hili limetokana na kushindwa kwa gharama za uchaguzi kuwa kubwa na hasa pale vyama husika kukosa pesa za kuweza kuwawezesha wagombea wao. 

HIVI NDIVYO MUDA UNAVYOPOTEA

KWA ASILIMIA KUBWA SANA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM TUNAPOTEZA MUDA MWINGI SANA KUKAA BARABARANI KWA AJILI YA FOLENI ZA ASUBUHI NA JIONI. KUTOKANA NA HILO UKUAJI WA KIUCHUMI NAO UKIZIDI KUDORORA. SERIKALI INABIDI ILITAZAME KWA UPANA ZAIDI ILI KUPUNGUZA TATIZO HILO. HIZO AHADI ZA KWENYE KAMPENI TUNAWAOMBA WAHESHIMIWA WAKIFANIKIWA WAZITIMIZE.....

MICHEZO HUJENGA AFYA

Nadya on slide
michezo kwa watoto huwapa uwezo wa kujiamini pindi wanapokutana na watototo wenzao. Pia michezo ni sehemu ya kuwajenga kiafya zaidi. Hivyo tuwape watoto zetu fursa za kuweza kuonyesha nini wanaweza fanya pindi wanapokutana na watoto wenzao

September 16, 2010

KARIBU ABAYA CENTRE-MAYFAIR PLAZA


Kwa mavazi ya uhakika kwa wakina mama na wasichana wa rika zote tembelea katika duka letu lililopo Mayfair Plaza maeneo ya Msasani karibu na Hospitali ya TMJ. Kwa mavazi, manukato na vito vya thamani fika na onana nasi.

September 08, 2010

Wafanyakazi wa Hindoo na Coast wakiwa mjengoni

MD- Abubaker Abubaker akizungumza jambo
WAZEE WA KAZI
Kutoka kushoto- Saada Azan(Coast Mlimani), Luiza Mahimbo(Coast Mlimani), Happiness(Coast mlimani) na Rukia(Hindoo Mayfair)
MD NA WAIFU  WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAFANYAKAZI WAKE
warembo wa Hindoo na Coast wakiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi
Wadau
Steve na mahakhui

Hii sio dua bali ni moja ya mikunjo ya kumaliza Futar- Sheikh Alawi

August 20, 2010

Hongera LYDIA BENDERA

Tunapenda kukupongeza sana sisi kama wanafamilia kwa kuweza kurudisha fomu zako na kuweza kupitishwa jina lako bila ya kupingwa. Hakika mwenyezi mungu yu pamoja nawe katika harakati hizi za kisiasa katika kuweza kuja kuwawakilisha vyema wapiga kura wako wa jimbo la Kibaha Mjini. Tunafahamu kuwa safari ni ngumu katika kuhakikisha ndoto zako zinakuwa lakini kwa uweza wake mola yote yatakuwa sawa. Hongera sana tena sana

August 16, 2010

Bi Bendera kupeperusha bendera ya CUF

Safari ni hatua wahenga walisema na ndivyo ilivyoanza kwa Bi. Lydia Bendera katika kinyang'anyiro cha kugombea ubunge katika jimbo la Kibaha Mjini huku akipeperusha bendera ya CUF. Kila rakheri katika harakati hizo.

July 10, 2010

Ni Dr Shein Zanzibar

Chama cha mapinduzi (ccm) kimemteua Makamu wa Rais, Dr Ali Mohammed Shein, kuwa mgombea urais wa zanzibar. Dr Shein amewaangusha wagombea 11 wa awali na kubakia wagombea watatu: Dr shein, Dr Mohammed Gharib Bilali na waziri kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha.

July 03, 2010

Balaaa jingine.... Germany VS Argentina

majonzi kwa Afrika


Majonzi makubwa sana kwa Waafrika karibu wote baada ya timu pekee toka katika bara la Afrika kutolewa jana katika michuano ya kombe la dunia katika mchezo uliochezwa jana katika uwanja wa Soccercity na timu ya Uruguay kwa kufungwa kwa njia ya penalt baada ya kuzecha kwa muda wa dakika 120.

June 14, 2010

CRDB WASTAHILI PONGEZI

Hakika benki ya CRDB inastahili pongezi kubwa hasa kwa kuzingatia kuwa muda ni mali. Kwa kulizingatia hilo benki imeweza kwa kiasi kikubwa kupunguza foleni ndani ya benki kwa kuweza kubuni njia mpya inayorahisisha wateja wake kufika dirishani kwa kuitwa kwa namba.kwa kulitimiza hili mteja anaweza kuwa na muda wa kufanya jambo jingine mpaka namba yake itakapotajwa.
Hongera CRDB KWA KUTHAMINI WATEJA WENU.

April 26, 2010

ombaomba wakitumiwa vizuri jiji letu litakuwa safi

Hebu jaribu kutazama nyuma ya pazia juu ya hawa ndugu zetu wasiojiweza ambao wamejitolea kuomba omba kwa watu wapitao barabarani. Hii imekuwa ni kero kwa wapitao na magari yao kwani imejitokeza tabia ya baadhi yao kufanya kinyume na lengo lao. Angalizo ninaloweza kusema ni juu ya uongozi wa jiji kuliangalia swala hili kwanza kama ni kero na pili kulitazama kama njia ya kuwapatia ajira. Hawa ndugu zetu wanaishi kwa muda mrefu sana barabarani jiji kitu cha kufanya nikuwawezesha kwa kuwapatia ajira ya kuliweka jiji safi nyakati za usiku na hivyo kuondoa ongezeko la ombaomba barabarani na pili kupungunza usumbufu kwa waendesha magari nyakati za asubuhi kukwepana na wafagiaji.

April 18, 2010

Simba Sports Club- Vodacom Premier League Champions 2009/2010

Vijana wa msimbazi Simba Sports Club wametangazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuikamilisha mechi iliyokuwa na shauku kubwa kwa kuwafunga watani wao wa jadi Yanga Dar African kwa mabao 4-3 mchezo uliochezwa katika dimba la uwanja mpya wa Taifa

March 19, 2010

Mauaji ya kikatili kwa maalbino yaiweka Tanzania pabaya

Mauaji ya kikatili kwa maalbino nchini Tanzania yameiweka nchi katika ramani mbaya hasa vipindi mbalimbali duniani kuonyesha unyanyasaji huo. kupitia kituo cha DISCOVERY CHANNEL siku ya alhamisi ya 25-03-2010 watarusha kipindi hicho kuhusu ukatili huo toka Tanzania

February 11, 2010

Babu Seya afungwa Maisha

Babu Seya na Papii Kocha kusota gerezani maisha. Katika hukumu iliyosomwa leo katika mahakama kuu na Jaji Neema.

February 10, 2010

HII NI AIBU...

Ule usemi wa mgeni njoo mwenyeji apone umejidhihirisha pale tunapoona barabara maeneo ya Leaders club ambayo yamekuwa ni maarufu kwa kutoa burudani mbalimbali hususani kwa wasanii wa ndani na nje ya nchi yetu. Lakini kwa kipindi kirefu sana tumekuwa tukishuhudia barabara mbovu iliyokuwa ikihatarisha uhai wa magari yetu. Serikali ilikuwa wapi? Au ndio ilikuwa wanasubiri ZINDUKA? Kama maendeleo yatakuwa yanasubiri ziara ya viongozi wa juu basi ile kauli mbiu ya ARI MPYA NGUVU MPYA NA KASI MPYA itakuwa kazi. Viongozi ZINDUKENI msimsubiri Rais

January 29, 2010

Inafaa hata hapa kwetu

Katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa Jiji la Dhaka, Bangladesh lenye wakazi wapatao milioni 20 wameanza kuweka vyoo vinavyotembea kwenye gari ili kupunguza matukio ya kujisaidia hovyo ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangia kuchafua jiji. Hapa kwetu tunashuhudia kuta mbalimbali zikiwa na matangazo yanayokataza watu kujisaidia 'TANGAZO HURUHUSIWI KUKOJOA HAPA AMRI'. Hivyo tunatoa changamoto kuwa katika ongezeko la kasi katika miji yetu mikuu kama Dar Es Salaam na kwingineko inastahili wakuu wa miji kuwa wabunifu ili kupunguza ama kuondoa tatizo hili.

January 25, 2010

hepi bethi dei cute NADYA

Hepi bethi dei Nadya.Dad, Mam and Rihanna wishing you all the happiness.

January 09, 2010

CAESAR & KADO WAMEREMETA


Ceasar na mai waifu wake Kado katika pozi

Mzee Stephen Mtaki na mai waifu wake Debora Salanya Mtaki (wazazi wa bi harusi) wakiwa na nyuso za furaha.

Kutoka kushoto ni mama Wanjiye(mama mkubwa wa bi harusi) na wazazi wa bi harusi

Kaka wa bi harusi.Emanuel-Salanya- Mtaki



Hakika ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa wawili waliopendana kwa dhati kutimiza ile ahadi ya mungu- Mathew 19:5-6. Hongereni sana

January 03, 2010

January 01, 2010

happy new year 2010

Wishing you all my friends a very happy new year 2010. Hope this year will have more and more to read. Thanks for your support.