February 10, 2010

HII NI AIBU...

Ule usemi wa mgeni njoo mwenyeji apone umejidhihirisha pale tunapoona barabara maeneo ya Leaders club ambayo yamekuwa ni maarufu kwa kutoa burudani mbalimbali hususani kwa wasanii wa ndani na nje ya nchi yetu. Lakini kwa kipindi kirefu sana tumekuwa tukishuhudia barabara mbovu iliyokuwa ikihatarisha uhai wa magari yetu. Serikali ilikuwa wapi? Au ndio ilikuwa wanasubiri ZINDUKA? Kama maendeleo yatakuwa yanasubiri ziara ya viongozi wa juu basi ile kauli mbiu ya ARI MPYA NGUVU MPYA NA KASI MPYA itakuwa kazi. Viongozi ZINDUKENI msimsubiri Rais

No comments: