September 20, 2010
RUSHWA KUISHINDA NI KAZI
Nimekuwa ni kijaribu kufatilia harakati hizi cha uchaguzi mkuu kwa ngazi ya Rais, Ubunge na udiwani unaotarajiwa kufanyika siku chache zijazo. Katika kutazama huku na kule nimekuja kubaini kuwa siasa kwa nchi zetu hizi za ulimwengu wa tatu hasa hivi vyama vya upinzani kuja kuondoa serikali kuu itakuja kuwachukua miaka kama si karne kuhakikisha wanachukua nchi. Tumeweza ona vyama vingi vikitoka jasho katika kuhakikisha kuwa wanaweza kuwafikia wananchi kwa kuelezea sera zao. Lakini kadiri siku nazo zilizivyokuwa zikienda vya vipinzani vimejikuta vikiuza nafasi zao kwa siri na kukiachia chama tawala. Na hili limetokana na kushindwa kwa gharama za uchaguzi kuwa kubwa na hasa pale vyama husika kukosa pesa za kuweza kuwawezesha wagombea wao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment