April 26, 2010
ombaomba wakitumiwa vizuri jiji letu litakuwa safi
Hebu jaribu kutazama nyuma ya pazia juu ya hawa ndugu zetu wasiojiweza ambao wamejitolea kuomba omba kwa watu wapitao barabarani. Hii imekuwa ni kero kwa wapitao na magari yao kwani imejitokeza tabia ya baadhi yao kufanya kinyume na lengo lao. Angalizo ninaloweza kusema ni juu ya uongozi wa jiji kuliangalia swala hili kwanza kama ni kero na pili kulitazama kama njia ya kuwapatia ajira. Hawa ndugu zetu wanaishi kwa muda mrefu sana barabarani jiji kitu cha kufanya nikuwawezesha kwa kuwapatia ajira ya kuliweka jiji safi nyakati za usiku na hivyo kuondoa ongezeko la ombaomba barabarani na pili kupungunza usumbufu kwa waendesha magari nyakati za asubuhi kukwepana na wafagiaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment