November 26, 2009
MITANDAO YA SIMU NA SOKO LA AJIRA
Katika kipindi cha hivi karibuni tumeshuhudia huduma za mitandao ya simu kuimarika kwa kiasi kikubwa hata kufanya huduma hiyo kuwafikia watumiaji wengi hapa nchini. Katika kuhakikisha matumizi ya huduma hiyo nyeti inawafikia walengwa kwa ubora wa juu makampuni yaliyo mengi nayo yamejikita katika kuhakikisha yanakwenda sambamba na soko la ushindani. katika hili wanastahili pongezi lakini kilichonifanya kuandika hiki ni juu ya makampuni haya kujihusisha na huduma za kifedha ambapo hapo awali zilikuwa zikifanywa na taasisi za kibenki. Wasiwasi wangu ni juu ya soko la ajira katika mabenki ambalo ndilo soko tegemezi kwa kiasi kikubwa kwa kuajiri watu wengi hususani wanafunzi pindi wamalizapo masomo yao vyuoni. Sasa kama huduma hii ya simu za mkononi itaweza kuwafikia watumiaji wa huduma hiyo kwa uhakika ina maana kuwa ajiri ya wafanyakazi walio katika taasisi za kifedha kama mabenki wakijikuta wanapoteza ajira zao. lakini je makampuni ya simu yamejiaandaa kukabiriana na wateja wao wote? Tunasikia kuwa makampuni hayo ya simu yanajianda katika kuhakikisha wafanyakazi wanapokea mishahara yao kupitia njia ya simu.Je usalama utakuwa je?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment