October 13, 2009

miaka 10 bila ya Mwl. J. K. Nyerere



Ni miaka kumi tangu mwl. J. K. Nyerere mwanzilishi wa taifa letu kututoka. Ni siku ya tarehe 14.10.1999 ndipo taifa lilipotwa na mshituko wa aliyekuwa baba wa taifa letu kipenzi cha watu kuwa ameaga dunia. Maswali mengi yalikuja vichwani mwa walio wengi juu ya namna taifa letu changa litakavyokuwa bila yeye. Japo mambo mengi aliyoyatabiri kuwa yatatokea kama yasiposhughulikiwa ndio yamejitokeza mfano ulimbikiziaji wa mali na mgongano wa kisiasa wa Zanzibar na mengine mengi. Imekuwa ni jadi yetu kama taifa kumkumbuka kila ifikapo tarehe 14. Je yale aliyoyaacha yanafuatwa? Viongozi wanakumbuka miiko ya uongozi? Mungu ilaze mahali pema roho yake amen.

No comments: